Kwa muda mrefu Christina Shusho ndiye amekuwa akitamba katika blogu hii kwa nyimbo na habari zake kusikilizwa na kusomwa sana. Hivi karibuni hata hivyo nyimbo za Mchungaji na mwimbaji mwenye kipaji cha pekee Solomon Mukubwa zimetokea kupendwa sana katika blogu hii na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Ukizisikiliza nyimbo hizi kwa makini, unaweza kuisikia sauti ya ndani kabisa yenye upako ikizungumza nawe. Kwangu mimi wimbo wa Mwamba Uliopasuka ndiyo natembea nao kila niendako na kila mara ninapousikiliza naguswa na nguvu za ajabu na kusogezwa karibu na Muumba wangu. Tunamtakia Mtumishi huyu wa Bwana kila la heri katika maisha yake mapya ya ndoa (soma hapa na hapa). Mungu Aendelee kumtia nguvu ili azidi kusonga mbele katika utumishi wake. Amen!
*********************
(1) MUNGU MWENYE NGUVU (NEEMA YAKE)
(2) MFALME WA AMANI
(3) MWAMBA ULIOPASUKA
(4) SIKU MOJA
(5) TABIA INA DAWA
(6) MKONO WA BWANA
(7) KIMBILIO LANGU
5 comments:
This is pure talent. Simply the best!!!
Mchungaji Solomon, Bwana Mungu Akubariki na kukulinda, wewe pamoja na familia yako! Nyimbo zako kila siku zina upako mpya!!!! Huduma yako ni njema mno!
Ni karama ya pekee!!!! Ni kipaji cha aina yake!!! Jina la Bwana Lisifiwe....!!!!
Mwamba uliopasuka...wimbo "umetuli!" Sauti za watumishi wa Mungu Solomon na Muliri zimepangiliwa vizuri mno! Mungu Awabariki na Kuwalinda, watumishi wa Mungu mtendao kazi yake bila kuchoka! Baraka kwenu!!!
Wimbo huu: NEEMA YAKE (ama Mungu Mwenye Nguvu, ama Ebenezer)!!!! Basi tu!!!
Hakika Baba Utukuzwe, Baba Uinuliwe…Uhimidiwe YAHWEH! Ni kweli, NENO lako linawafungua watu kutoka katika vifungo mbalimbali vya shetani! Hakika Baba rehema zako ni mpya kila siku! Tulimpa nini Mungu hata twaamka salama, kama si neema yake tu?? Kama lipo la kujivunia, basi twajivuna katik aKristo Yesu tu…! Asante sana mtumishi wa Mungu, Solomon! Kwa mahubiri haya Bwana Mungu Akubariki sana.
Post a Comment