Mkali wa Muziki wa Injili Bongo, Christina Shusho amepangua vikali madai yanayovumishwa kila kona ya jijini la Dar kuwa, amekuwa na kijitabia cha kutapanya fedha zake vibaya kwa kufanya matanuzi ambayo kwa hadhi yake hapaswi kuyatenda.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Shusho alisema kuwa, anashangazwa na uvumi huo ambao hauna ukweli wowote bali una lengo la kuinajisi huduma yake ili aeleweke vibaya katika jamii.
“Si kweli kwamba mimi nafanya matanuzi kwa kutumia fedha kama watu wanavyodai, bali naona watu wameamua kunichafua kwa maneno ya uzushi ili jamii inichukie ikiwa sambamba na kuinajisi huduma yangu,” alisema Shusho ambaye ni miongoni mwa waimbaji wachache wa muziki huo ambao wamekuwa wakihesabika kuwa ‘wasafi’.
Mbali na matumizi mabaya ya pesa, msanii huyo anadaiwa kulala kwenye hoteli za nyota 5 punde anaporejea jijini usiku akitoka kufanya shoo zake mikoani.
Akipangua skendo moja baada ya nyingine, Shusho alikiri kwanza kuwa na safari za kwenda kununua nguo zake nje ya nchi akisema kwa sababu ana duka la nguo Kariakoo.
Aidha, alisema kuwa, yeye ni mwanamitindo hivyo anapokwenda Marekani, Uingereza au China hununua vitambaa ambavyo vikishonwa na kuvaa huonekana amenunua nguo za gharama kubwa.
“Mimi ni mtu ninayetumika madhabahuni, natakiwa nionekane nadhifu muda wote, na kweli nimekuwa nikisafiri kwenda Ulaya kununua bidhaa za dukani kwangu, na nikiwa huko huwa nanunua kitambaa kimoja kimoja, nikija kushona nguo na kuvaa zinaonekana nzuri na za gharama ya juu na baadhi ya watu hutafsiri kwamba, natumia vibaya fedha zangu,” alisema Shusho.
Akifafanua kuhusu suala la kulala hoteli za gharama nchini anaporeja Dar usiku toka kwenye shoo, Shusho alisema kuwa, jambo hilo halina ukweli wowote kwa sababu ana mapenzi na familia yake hivyo hawezi kufanya kitendo kama hicho.
Mwimbaji huyo alimaliza kwa kusema kuwa, yote hayo anamwachia Mungu yeye ndiye anayejua ukweli wa maisha yake, na masuala hayo anayapeleka kiroho zaidi kuliko kimwili kwani yanaweza kuujeruhi moyo wake.
“Namwachia Mungu masuala hayo, yeye ndiye anayefahamu ukweli wa maisha yangu kwa maana Biblia inasema; Kushinda kwetu si kwa damu na nyama bali ni katika Ulimwengu wa roho, Jehova atalidhibitisha jambo hili kama lipo, na kama halipo wanaovumisha maneno hayo atawashughulikia,” alisema Shusho.
****************************
Angalizo la Nyimbo za dini blogu: Kuna skendo gani hapa? Kama Christina Shusho amezipata hizi pesa kwa njia ya halali, basi ni zake na ana uhuru wa kuzitumia vyo vyote anavyotaka. Hayo mambo ya kusaidia mayatima na wenye matatizo, kutoa zaka na mengineyo ni kati yake na Mungu wake. Ukisoma Biblia vizuri mambo haya yanapaswa kutendwa kwa siri. Kama hivi ndivyo, tunajuaje kama Shusho hawasaidii mayatima na wenye shida? Au kwa vile amelala katika hoteli ya nyota tano? Kulala kwenye hoteli ya aina hii ni kosa? Christina - unacho kipaji cha pekee katika uimbaji. Makinikia kazi yako uliyoitwa kuifanya hapa duniani na mengine yote ni madogo. Binadamu watasema katika kila jambo utakalotenda. Walimwandama Yesu sembuse wewe? Usikatishwe tamaa bali pigana vita vilivyo imara vya imani. Tunakuombea!!!
5 comments:
shusho yuko juu. eabarikiwe wote wanaoifanya kaz ya Mungu aliyeziumba mbingu na nchi kwa moyo. KWA YESU KUNA RAHA
KAMA NI MATUMIZI YA PESA, TUMIA TU SHUSHO KWANI UNAZITAFUTA MWENYEWE ILA ANGALIA ZISIKUTENGE NA UWEPO WA YEHOVA. NYIMBO ZAKO NZURI KWA KWELI WATU WENGI TUNABARIKIWA NAZO KWANI ZINATUSOGEZA MBELE YA UWEPO WA MUNGU. YESU NDIYE MSAADA WETU TUOMBE LOLOTE KWA JINA LAKE HUKU TUKIAMINI NASI TUTAPOKEA. AMEN
NAKUMBUKA VILE ULIVYOTUTEMBELEA KICC HAPA KENYA ,NA MIMI NI CHRISPINE ODHIAMBO FROM NAIROBI NILIYEKUPIGIA SIMU (0717326464)SAFARICOM''LAKINI ILIKATA ONLINE ,MUNGU AMEKUCHUNGA KWA MFANO WA YESU ALIE ZALIWA KWA KUWAOKOA WATU WOTE HAPA DUNIANI NA MUNGU AZINDI KUKUPONYA.
JULIUS.SAID SHUSHO YOUR SONGS ARE BLESSING ME SOO MUCH AND YOUR HIGH.TO USE MONEY IS NOT PROBLEM AND NO ONE IS ALLOWED TO JUDGE YOU ABOUT HOW YOUR USING YOUR MONEY EXPECT GOD HIMSELF.THROUGH YOUR SONGS PEOPLE ARE SAVED AND HEALED
SHUSHO UNANIBARIKI SANA.HASA NIKIKUMBUKA WIMBO WA MTETEZI WANGU YU HAI.NILIPOMALIZA FORM SIX 2008 ULINITIA MOYO NIKAONA KWELI MTETEZI
Post a Comment