Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Tuesday, March 9, 2010

WAPENDWA, MNAONAJE TUKIFANYA HIVI?

Wapendwa na wakereketwa wa blogu hii

Ati, mnaonaje tukikusanya nguvu zetu pamoja kwa kuweka audio za nyimbo zetu za dini tulizonazo mahali pamoja yaani katika blogu hii? Mnaonaje kama kila mmoja wetu akinitumia nyimbo tano (audio) za injili azipendazo? Baada ya kukusanya nyimbo zote, mimi nitatengeneza player moja nzuri kama hiyo ya nyimbo za Ulyakulu hapo kulia na kuiweka hapa? Kwa jinsi hiyo tutakuwa na nyimbo zaidi ya 500 za injili sehemu moja. Mimi nitajitolea kulipia gharama zote za kununulia bandwidth na kuhakikisha kwamba player yetu inafanya kazi muda wote. Nyinyi mnaonaje? Mimi nadhani hili ni wazo zuri.

Unachotakiwa kufanya ni ku-zip nyimbo tano za injili uzipendazo sana na kunitumia kupitia limbejuma@gmail.com.

Hii ni blogu yetu sote na mawazo mengine ya jinsi ya kuiendeleza yanakaribishwa.
Mungu Aendelee kutubariki.

2 comments:

Yohana Limbe Juma (Mtumishi) said...

Asante sana dada Rhoda (Norway) kwa nyimbo zako ulizotuletea. Ni wewe pekee uliyeitikia ombi hili. Asante sana na Mungu Akubariki sana!

MBOGELA, Jackson said...

Naunga mkono Hoja kama tunaweza kupata Audio itatusaidia sana, wakati mwingine kwenye sherehe hasa kwa wale walioko nje ya nchi kama ulaya na Marekani wakati mwingine wanahitaji kupiga nyimbo za nyumbani moja kwa moja toka kwenye player iliyoko online bado kuna shida, player zilizopo mpaka sasa hazina nyimbo nyingi na haziwi updated mara kwa mara. Mtumishi kama nitapata nyimbo yoyote nitakutumia,