- Kumekuwa na jambo linalokera kwa baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili, kuna nyimbo nyingine hata sisikilizi wala kuangalia, hata wewe mpendwa ikiwa umeokoka ukiziona hizo nyimbo utasikitika, hazina Utukufu hata kidogo, hazina tofauti na nyimbo za “Misri” wanavyoimba na kucheza kama vile hawako serious na uimbaji wa nyimbo za Injili. Kama vile wanajiimbia wao na kuwaburudisha wanaowasikiliza.
- Unaposema unaimba nyimbo za Injili, sio kwa sababu una pesa ya kuingia studio na una sauti nzuri. Watu wengi tunapenda kusikiliza nyimbo za Injili ili tuone mabadiliko kwenye maisha yetu sio kutuburudisha, angalia tungo zako zimekaaje, wengine wakisikia neno limeingia mitaani, tayari wamepata kichwa cha habari cha wimbo! Usafi wa moyo ndio unadhihirisha kazi yako. Mungu akubariki muimbaji wa Injili naomba unisamehe kwa makwazo yangu. Nawakilisha!
–Jonas Malimbo–
Chanzo: Strictly Gospel.
No comments:
Post a Comment