- Mtumishi wa Mungu mwenye uwezo mkubwa wa kuhubiri Neno Bishop Eddie Long (na mpinzani mkubwa wa mahusiano ya kishoga) mambo yamembumburukia (kama wenzake hawa) baada ya kushushiwa tuhuma nzito na wavulana wanne ambao walikuwa waumini wa kanisa lake. Wavulana hawa tayari wameshafungua kesi mahakamani na mwingine wa tano anategemea kufanya hivyo hivi karibuni.
- Wavulana hawa wanadai kwamba Bishop alikuwa akiwalaghai kwa pesa, magari, vito vya thamani na safari za ndani na nje ya Marekani huku akijifanya kuwa kama "baba" kwao na baadaye kutumia nafasi hiyo kuanzisha uhusiano wa kingono.
- Habari hizi zipo kila mahali hapa Marekani na sasa kuna picha ambazo zinadaiwa kwamba Bishop alikuwa akiwatumia vijana hawa na "text messages" ambazo alikuwa akiwaomba pia wamtumie picha zao. Na kwa wanaopenda kuhukumu, tayari wameanza kupaza sauti wakidai ni lazima ajiuzulu wadhifa wake kama Mchungaji Mkuu wa kanisa kubwa la New Birth Missionary Baptist Church lenye waumini wapatao 25,000 wakiwemo watu mashuhuri mbalimbali.
- Watu wengi wanatumaini kwamba tuhuma hizi ni za uwongo na pengine wavulana hawa wanataka pesa. Lakini kwa vyo vyote vile hili si jambo jema. Mungu Atusaidie sote na kutupa rehema zake ambazo bila kwazo kamwe hatuwezi kuokolewa! Tukumbuke kwamba hakuna aliye mkamilifu.
No comments:
Post a Comment