- Kama ambavyo tuliwahi kuandika hapa juu ya uchumba wa Upendo Nkone - mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, harusi yake sasa imewadia. Mtumishi huyu wa Bwana anatarajia kufunga ndoa na Mchungaji John Mbeyela oktoba 17 mwaka huu.
- Habari zilizopatikana kupitia gazeti la Majira zinaeleza kwamba Upendo Nkone ataagwa nyumbani kwao Kigoma Oktoba 11 na ndoa yake na mchungaji huyo ambaye naye ni mjane mwenye watoto watatu itafungwa katika kanisa la Naioth maarufu Kwa Mwasota lililopo Mabibo Makuburini jijini Dar es salaam.
- Mwimbaji huyo mashuhuri alianza kuimba miaka mitano iliyopita na mpaka sasa amefanikiwa kutoa albamu tatu ambazo ni Mungu Baba, Hapa Nilipo na Zipo faida.
- Mtumishi, tunakutakia kila la heri katika ndoa yako
No comments:
Post a Comment