Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Tuesday, March 22, 2011

ETI, KUTUMIA LUGHA YENYE KUONYESHA USAWA WA KIJINSIA KATIKA BIBLIA (ZA KISASA) NI "KUCHAKACHUA" NENO LA MUNGU?

Kwa tunaoamini kwamba Biblia ni neno la Mungu, ni sawa kweli kuibadilishabadilisha mara kwa mara ili lugha yake iendane na wakati uliopo na mazingira tuliyomo? 

Swali hili limezuka baada ya wafasri wa toleo jipya la mwaka huu la Biblia inayopendwa sana ya New International Version Bible (NIV) kuamua kutumia lugha inayoakisi usawa wa kijinsia. Kwa mfano, badala ya kusema, "If anyone says, 'I love God,' yet hates his brother, he is a liar.", sasa Biblia hiyo inasomeka "If anyone says, "I love God,' yet hates his brother or sister, he is a liar."

Kuna wanaodai kwamba Biblia ni neno la Mungu na kamwe haipaswi kuwa inabadilishwabadilishwa kila mara mikondo au matapo ya mawazo yanapobadilika  katika jamii kwani kwa kufanya hivyo itafikia mahali tutakuwa tunapotosha kabisa maana iliyokusudiwa. Wewe unasemaje kuhusu suala hili?

Kwa habari zaidi kuhusu utata huu wa tafsiri bofya HAPA (Tazama maoni mengi yaliyotolewa hapo). Unaweza pia kusoma kitabu kinachochambua japo hili kwa kina HAPA (pdf - kurasa 357)

4 comments:

Anonymous said...

Inategemea...kwingine ni Jewish influences tu ambazo zinamkandamiza mwanamke, na hizo zaweza kuonekana hata kwenye "namna" ya uandishi. Uunapojaribu kuondoa hizo elements za Jewish culture katika Biblia unaonekana unachakachua Neno la Mungu!

Anonymous said...

Inategemea...kwingine ni Jewish influences tu ambazo zinamkandamiza mwanamke, na hizo zaweza kuonekana hata kwenye "namna" ya uandishi. Uunapojaribu kuondoa hizo elements za Jewish culture katika Biblia unaonekana unachakachua Neno la Mungu!
Joseph Nyemi, Arusha

Anonymous said...

Anony - tutajuaje kuwa ni Jewish influences tu? Anyway, Bible ni mkusanyiko wa hekaya (fables) za KiJew and I don't have any problem hata ikibadilishwa namna gani. They are just stories sawa na zile za makabila yetu.

Anonymous said...

Mwanangu, hapa umerusha kete nzuri na yenye kutia changamoto sana katika maisha ya waumini wa ki-Kristo! Lakini kwa harakaharaka mfano ulioutoa katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili unaleta mvuto wenye mantiki fulani. Lakini tukumbuke kuwa Biblia iliandikwa na waandishi mbalimbali na wakiwa katika muktadha tofauti. Kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili, mkono wa kulia mara nyingine huitwa "mkono wa kuume" na "Mungu Baba". Kwa mantiki hiyo sehemu fulani ya Biblia inasemwa kwamba wale watakaokombolewa wataketi katika mkono wa kuume wa Mungu na wala si katika mkono wa kike wa Mungu.

Mtu anaweza kudiriki kusema kwamba labda wakati wa uandishi wa Biblia mfumo-dume ulikuwa umeshamiri sana kwa maana hata wanazuoni wa wakati ule walikuwa ni wanaume kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo mwanazuoni maarufu katika Agano la Kale, Mtume Petro, anasema kwamba ujumbe wote ulioko katika Biblia haujawekwa kwa matakwa ya mwanadamu bali watu wote waliohusika na uandishi wa ujumbe huo walikuwa wamevuviwa Roho Mtakatifu (2Pet.1:20-21). Imefika muda sasa tutasema, na tayari wanawake wameanza kuhoji, ni kwanini Yesu aliteua mitume wa kiume tu?

Haya marekebisho inabidi yafanywe kwa hekima ya kimbingu vinginevyo watu wataanza kuhoji hata vitu visivyo na msingi, kwa mfano, "mbona mimi niliumbwa nikiwa mwanaume?" nakadhalika nakadhalika. Kwa kuhitimisha mimi nasema kwamba Biblia haiwabagui wanawake wala wanaume bali sisi wenyewe tunajibagua.