Wasanii watamba kupagawisha kesho
Imeandikwa na Mwandishi Wetu
Tarehe: 22nd Aprili 2011
WASANII watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka wametamba kuwa kesho watatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki watakaojitokeza.
Tamasha la Pasaka litafanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kisha Jumatatu Uwanja wa Jamhuri Dodoma na Jumanne Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi yote muhimu yamekamilika na kuwa karibu wasanii wote muhimu tayari wameshafika Dar es Salaam.
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Msama, inawakariri wasanii mbalimbali wakizungumzia tamasha hilo, huku wakitamba kwamba mambo yatakuwa mazuri kesho.
“Nimedhamiria kuwapa mambo mazuri mashabiki wangu, najua watafurahi sana, watakaokuja hawatajuta,” ni kauli ya Rose Muhando.
Naye msanii Upendo Nkone, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwa wana imani kubwa litakuwa tamasha la kufunga mwaka.
Wasanii wengine wa Tanzania ambao pia wamezungumzia tamasha hilo ni Martha Mwaipaja, Christina Shusho na Boniface Mwaitege, kila mmoja akitamba mashabiki watafurahi.
Wasanii wa nje ya Tanzania ambao pia wamezungumzia tamasha hilo ni Annastazia Mukabwa, Solomon Mukubwa, Pamera Wanderwa na Geraldine Odour kutoka nchini Kenya.
Wengine watakaotumbuiza kesho ni Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayetamba na kibao cha Hakuna Kama wewe na Ephraem Sekeleti kutoka Zambia.
Chanzo: Habari Leo
~~~~~~~~~
3 comments:
Mbona hubadilishi Posti zako ndugu yangu. Nyimbo za ABIUD MISHOLI Zina zaidi ya miaka miwili sasa wakati kuna Video nyingi mpya zinatoka. Tafadhali nenda na wakati, blog yako hii ni muhimu sana.
Ndugu Anony - Nakuelewa. Siko Tanzania na siyo rahisi rahisi kupata nyimbo mpya. Kila kitu kilichoko hapa nakipata kutoka Youtube.
Kama wewe unazo hizo nyimbo mpya zilete nasi tutaziweka hapa.
Isitoshe: Mimi naamini kwamba neno la Mungu huwa halizeeki; na hata kama ni nyimbo za zamani, ujumbe wake unabakia ule ule.
Asante na Mungu Akubariki sana !!!
Bwana Yesu asifiwe,pole na kazi.Kaka ninakuomba unisaidie kuilink website yangu kwenye blog yako,ni website inayoitw www.nationalnetworkofprayer.webstarts.com ni website ya mtandao wa maombi,naomba unisaidie kuitangaza kaka.by Brown-0757-000039
Post a Comment