Waingereza wana msemo kwamba "You must stand for something or you will fall for anything"
Ati, linapokuja suala la imani na maisha yako ni nini ambacho huwezi kukitenda kamwe kabisa kabisa hata kama ungeahidiwa utajiri, umaarufu na mamlaka? Kuwa na msimamo katika maisha ni jambo la muhimu sana kwani ndilo linaonyesha kwamba binadamu tuna utashi - na hii ndiyo tofauti kubwa kati yetu na wanyama wengine. Kwa mantiki hii, mtu asiyekuwa na msimamo hana tofauti na wanyama wengine na pengine hastahili hata kuitwa binadamu.
Ngoja niulize tena:
Una msimamo katika maisha yako?
Ni jambo gani ambalo kamwe kabisa huwezi kulitenda hata iweje?
Ni kuua? Ni kuzini? Ni kufisadika? Ni nini?
Tafakari!
Una msimamo katika maisha yako?
Ni jambo gani ambalo kamwe kabisa huwezi kulitenda hata iweje?
Ni kuua? Ni kuzini? Ni kufisadika? Ni nini?
Tafakari!
No comments:
Post a Comment