Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Monday, September 14, 2009

KIRK FRANKLIN ALIPOTEMBELEA UGANDA

Kwa mnaokerwa na Steji shoo za waimbaji wetu wa nyimbo za injili, mtazameni Kirk Franklin - mwimbaji mashuhuri sana wa nyimbo za Injili kutoka Marekani. Hapa alikuwa Uganda akieneza neno la Mungu. Hoja ni kwamba kama tunataka kuwavutia vijana kumwamini Mungu ni lazima tuwafuate huko huko waliko - kwenye miziki yao ya kufokafoka, tuige uchezaji wao pamoja na mambo yao ya kijanajana. Sijui kama mtazamo huu ni sahihi ama la lakini inatia hatihati kidogo kuona kwamba kanisa inabidi lijishabihishe na mambo ya kidunia na si kinyume chake. Kanisa kuonekana la kizamani na lisilokifaa kizazi kipya ni sababu mojawapo inayotajwa kwamba imesababisha kufifia kwa Ukristo katika sehemu nyingi za Ulaya kiasi kwamba makanisa mengi yanafungwa. Steji shoo kama hii ya Kirk Franklin mnaionaje? Ni sawa makanisani?

3 comments:

Wilson Godfrey (Mbeya) said...

Ukristo hapa ndipo unapopoteza mwelekeo kabisa. Mbona uisilamu leo ni dini inayoenea kwa kasi sana Ulaya na Marekani? Je, kuna haya mambo ya rap na huu upuuzi mwingine katika Uisilamu? Ukifanya haya mambo anayofanya huyu Kirk Franklin hapa kwenye uisilamu utapigwa mawe. Ukristo umejiachia mno na ndiyo maana kwa wengine unaonekana kama dini isiyo na mwelekeo. Tazama kwa mfano Biblia. Leo hii naweza kukaa chini na kuandika version yangu ya Biblia (Wilson's Bible) na kubadilisha vile ninavyotaka. Yaani kuna Biblia unasoma unashangaa kama ni Biblia ile ile. Hebu jaribu kufanya hivyo kwenye Korani uone. Ukristo unapoteza mwelekeo na kama tutaendeleza haya mambo basi sijui tunaelekea wapi. Natumaini na wengine mtachangia!

Anonymous said...

Ukristo ni dini isiyo na wenyewe ndiyo maana hata huoni watu wakijadili hili jambo la muhimu. Sijui tu Wakristo tukoje. Ingekuwa ni site ya Waislamu wangekuwa mbele sana kujadili mambo yanayohusu dini yao. Lakini Wakristo mhhhh....

joseph india said...

unajua kwakweli mimi ni mkrisho hila kuna mambo ambayo kwa sasa tumezidi kuwa watu wa YES na ndio maana naona ulaya sasa makanisa yamegeuka kuwa malls,au makumbusho tu, kwa kuwa matukio mengi sana yanafanyika tunaenda nayo na wakati km hili la kucheza nyimbo za dini km dansi na hata uvaaji makanisanibaadhi ya dadazetu na uhuru usio na kipimo nao ukizidi ni hasara sana kwenye jamii
waislam wanakuwa wakali kwenye dini yao na hata msimamo wao wa kutobadibadilisha kitabu chao korani unafanya uislamu uwe makini sana kwavile bible ya zamani na ya sasa kwakweli ni tofauti sana za sasa zimejaa maandiko yasiyokuwepo.
mfano mi nakumubuka babu yake baba aliwahi kuniambia kuwa bible ilikuwa na maandishi ukiombewa na hiyo mistari unaweza kukauka huku ukicheka, na bible ilikuwa takatifu kiasi kwamba ukiishika na kulala nayo kule kijijini hata ndege aina ya bundi aji kwako wala mapepo ayawezi kuja
hila sasa sijui kwa wenzangu.
pili haya mambo ya kwenda na wakati ndio yamechangia sana maana leo kuna makanisa yanahubiri USHOGA wazi wazi na vitendo vingi viovu vya kulawiti vinafanywa na wachungaji au viongozi wakubwa wa dini.
Dini yetu sasa imekuwa biashara kubwa wengi wanaubiri pesa tu na si neno la mungu
yaani mi namuomba sana YESU arudi huku duniani kwavile alisema atakuja tena
fikiria leo kuna YESU huko urusi na amepata wafuasi wengi tu wa kikikristo NA wakati huohuo kuna jamaa akajifanya mtume wakamuua muda huohuo waislamu na huyo YESU yupo mpaka leo
mi nasadiki kuwa karne ya 19 ukristo ndio ulianza kudidimia baada ya mafisadi kujifanya wachungaji na wanamjua sana mungu
ni hayo hila nina mengi ya kusema
naona tu nitamkufuru mungu wangu kupitia yesu kristo