MAHUBIRI YA MZEE WA UPAKO NA MTUME/NABII JOSEPHAT MWINGIRA

Mahubiri ya Mzee wa Upako

Mahubiri ya Mtume na Nabii Josephat Mwingira

Thursday, September 3, 2009

ATI, STEJI SHOO KATIKA NYIMBO ZA INJILI NI SAWA?

Kuna watu ambao wanakerwa na steji shoo kabambe ambazo zinaambatana na nyimbo za dini siku hizi. Kuna wanaodai kwamba katika uchezaji na mikikimikiki inayoambatana na uchezaji huu (ambao mwingine unazidi kiasi na kuonekana kuwa kama muziki wa kidunia japo maneno ni ya kumsifu Mungu) watu wanakaza fikra zao kwa wacheza shoo badala ya kusikiliza ujumbe katika nyimbo. Na hii inapoteza dhana nzima na kusudi hasa la nyimbo za dini. Steji shoo nyingine zinaambatana na matangazo ya makampuni ya biashara yaliyotoa udhamini kama Coca Cola, Vodacom n.k. Ati, ni kweli kwamba steji shoo hizi zinatia dosari katika utumishi wa waimbaji wa nyimbo za injili? Au ni mitindo isiyoepukika hasa wakati huu wa utandawazi ambapo kila kitu ni BIASHARA?

(1) ROSE MUHANDO(2) UPENDO NKONE


(3) WANAKUNYATA


(4) BONY MWAITEGE

(5) CHRISTINA SHUSHO

1 comment:

John Mwaipopo said...

Mie nafikiri ni sawa lakini show zisivuke mipaka tu.