- Mashujaa wa imani wa kike wanaendelea kujitokeza na kujitoma shambani mwa Bwana kuchapa kazi. Huyu hapa ni Mchungaji wa Kitanzania anayesomea shahada ya uzamifu (Ph.D) katika taaluma ya Thiolojia kule Norway akigawa mibaraka ya Bwana kule Karege Matumbi (nje ya Bagamoyo). Nyimbozadini.blogspot.com inawapongeza akina mama wote wanaojitoma shambani mwa Bwana kwani mavuno ni mengi lakini wavunaji ni wachache. Mungu Aendelee kuwabariki na kuwatumia kama Anavyotaka. Amen!


