Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili
Showing posts with label KUTOKA STRICTLY GOSPEL. Show all posts
Showing posts with label KUTOKA STRICTLY GOSPEL. Show all posts

Sunday, April 17, 2011

Mwingira Amtangazia Kifo Babu wa Loliondo


- Adai siku zake za kuishi zinahesabika

Kiongozi mkuu wa huduma ya Efatha, Mtume na Nabii Josephat Mwingira amemtangazia kifo Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila, maarufu kama Babu wa Loliondo, huku akisema siku za babu huyo kuishi sasa zinahesabika.

Akitoa tangazo hilo mbele ya waumini katika makao makuu ya huduma hiyo Mwenge, jijini Dar es salaam, Jumapili iliyopita, Mwingira alisema babu Mwasapila atakufa kwa kuwa amemtukana Mungu wa Mwingira kwa kuzidi kutamka kuwa tiba anayoitoa imetoka kwa Mungu.

Mwingira ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu tangu atangaze rasmi vita dhidi ya Babu Mwasapila. Akitangaza vita  hiyo, Mwingira aliilaani tiba ya Babu huku akisema; “itoweke na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti”

Katika tukio la Jumapili iliyopita, mwingira alisoma andiko kutoka Waebrania 1:1-2, kisha akasema Mungu haongei na miti huongea na wanadamu ambao ni watumishi wake. Aliendelea kusema kuwa, babu wa Loliondo amemkasirisha sana kwa kuwa amemtukana Mungu kwa kusema kwamba Mungu ameongea na miti na badala ya watumishi wake.

“Mungu haongei na miti, anaongea na watumishi wake, hata katika kuponya Mungu ameagiza tuweke mikono kwa wagonjwa, Marko 16:15-18 inafafanua hili. Sasa kwa sababu babu wa Loliondo amemtukana Mungu, naye siku zake zinahesabika, kwani Biblia inasema usimwache mchawi kuishi” alisema Mwingira.

Wakati akiendelea na mahubiri yake huku akipita kuombea wenye shida mbalimbali, ghafla alifuatwa na mtumishi mmoja wa kanisa hilo na kumweleza kuwa, ndani ya kanisa hilo amekamatwa msichana ambaye ametumwa kuloga ili kuharibu kazi ya Mungu.

Hata hivyo, Mwingira hakuonesha kushtushwa na taarifa hiyo badala yake aliendelea kuombea watu huku akisema; “mimi sitishwi na wachawi” baadaye wakati akiendelea kuombea watu waliofika eneo ambalo msichana huyo alikuwa ameanguka na kuamuru ainuliwe ili amhoji.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa msichana huyo ni wapi alikotokea na alikuwa ametumwa na nani. Katika majibu yake msichana huy0 alieleza kuwa ametokea Ngorongoro na ametumwa na mtu aliyedai amechoshwa na maombi ya Mwingira yanayokwamisha kazi zake za kichawi. Msichana huyo alitaja jina la aliyemtuma ambaye hatuwezi kuandika jina lake.

Msichana huyo alikutwa na pete yenye picha ya mtu aliyetajwa na msichana huyo kuwa ndiye kamtuma, pamoja na chuma kilichochongwa mfano wa fuvu lililobebwa na ndege pamoja na bangili kubwa ya shaba.

Baadaye Mwingira alimuuliza; “sasa nikufanye nini”? yule msichana akajibu; “naomba unisamehe sitarudia tena ufanya uchawi na sitarudi kule nilikotoka” Mwingira akamuuliza tena; “Unakubali kumpokea Yesu”? yeye akajibu; “ndiyo” Baadaye msichana huyo aliongozwa sala ya toba.

Mwingira ni mmoja wa viongozi wa dini ya kipentekoste ambao walikuwa wa kwanza kabisa kutangaza kuipinga tiba ya Babu wa Loliondo.

Kwa habari zaidi kuhusu babu wa Loliondo, bofya HAPA

Monday, November 29, 2010

"NIPE MACHO" YA CHRISTINA SHUSHO IKO MITAANI


Muimbaji wa Nyimbo za Injili Christina Shusho tayari Album yake ya tatu NIPE MACHO iko mitaani, album yake ina jumla ya nyimbo kumi 1. NINA WIMBO. 2. BADO NAKUNGOJA 3. MUNGU UHIMIDIWE 4. NIPE MACHO 5. MAPITO 6. MUNGU AKIWA 7. THAMANI YA WOKOVU 8. NI KWA NEEMA 9. USHIRIKI NA ROHO 10. MUNGU WA HURUMA.

—Jipatie Nakala Yako—

Habari hii ni kutoka Strictly Gospel.

Kuna aliye na wimbo angalau mmoja tu atuonjeshe???

Thursday, August 19, 2010

ETI, UKATOLIKI NI UCHAWI? - MJADALA MKALI UNARINDIMA KULE STRICTLY GOSPEL

  • Kuna mjadala mkali unarindima kule Strictly Gospel. Mtu mmoja ameandika kitabu kinachothibitisha kwamba dini ya kikatoliki ni dini ya "kichawi". Mpaka sasa watu 70 wameshatoa maoni yao, na maoni mengine ni ya kina na yenye kufungua macho. Mada na mjadala huo vinapatikana hapa.
  • Sisi nyimbozadini.blogspot.com hatubagui dini wala dhehebu la mtu ndiyo maana hapa tunaweka nyimbo za aina yo yote ali mradi tu zinamtukuza Mungu. Tunaamini kwamba hatupaswi kuhukumu na mwenye uamuzi wa mwisho nani anakwenda mbinguni au motoni ni yeye aliyetuumba. Dhehebu linaokoa???

Friday, July 9, 2010

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI IMBENI NYIMBO ZA KUMWINUA KRISTO

  • Kumekuwa na jambo linalokera kwa baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili, kuna nyimbo nyingine hata sisikilizi wala kuangalia, hata wewe mpendwa ikiwa umeokoka ukiziona hizo nyimbo utasikitika, hazina Utukufu hata kidogo, hazina tofauti na nyimbo za “Misri” wanavyoimba na kucheza kama vile hawako serious na uimbaji wa nyimbo za Injili. Kama vile wanajiimbia wao na kuwaburudisha wanaowasikiliza. 
  •  Unaposema unaimba nyimbo za Injili, sio kwa sababu una pesa ya kuingia studio na una sauti nzuri. Watu wengi tunapenda kusikiliza nyimbo za Injili ili tuone mabadiliko kwenye maisha yetu sio kutuburudisha, angalia tungo zako zimekaaje, wengine wakisikia neno limeingia mitaani, tayari wamepata kichwa cha habari cha wimbo! Usafi wa moyo ndio unadhihirisha kazi yako. Mungu akubariki muimbaji wa Injili naomba unisamehe kwa makwazo yangu. Nawakilisha!
 –Jonas Malimbo

Chanzo: Strictly Gospel.

Monday, April 6, 2009

AINA GANI YA MUZIKI UNAFAA MAKANISANI?

Tembelea link ifuatayo kwa mjadala mkali kuhusu aina ya Muziki unaofaa makanisani. Asante dada Joyce kwa link hii. Ni mjadala mrefu wenye kufunua macho. Mungu aendelee kutubariki

http://strictlygospel.wordpress.com/2009/02/26/aina-gani-ya-muziki-wa-injili-unafaa-makanisani/