Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili
Showing posts with label KIRK FRANKLIN. Show all posts
Showing posts with label KIRK FRANKLIN. Show all posts

Monday, September 14, 2009

KIRK FRANKLIN ALIPOTEMBELEA UGANDA

Kwa mnaokerwa na Steji shoo za waimbaji wetu wa nyimbo za injili, mtazameni Kirk Franklin - mwimbaji mashuhuri sana wa nyimbo za Injili kutoka Marekani. Hapa alikuwa Uganda akieneza neno la Mungu. Hoja ni kwamba kama tunataka kuwavutia vijana kumwamini Mungu ni lazima tuwafuate huko huko waliko - kwenye miziki yao ya kufokafoka, tuige uchezaji wao pamoja na mambo yao ya kijanajana. Sijui kama mtazamo huu ni sahihi ama la lakini inatia hatihati kidogo kuona kwamba kanisa inabidi lijishabihishe na mambo ya kidunia na si kinyume chake. Kanisa kuonekana la kizamani na lisilokifaa kizazi kipya ni sababu mojawapo inayotajwa kwamba imesababisha kufifia kwa Ukristo katika sehemu nyingi za Ulaya kiasi kwamba makanisa mengi yanafungwa. Steji shoo kama hii ya Kirk Franklin mnaionaje? Ni sawa makanisani?