Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili
Showing posts with label BAHATI BUKUKU. Show all posts
Showing posts with label BAHATI BUKUKU. Show all posts

Tuesday, April 8, 2014

Wapendwa; Nimerudi na Blog Hii Itafufuka Tena. Karibuni Upya Ili Tuendelee Kumtumikia Mungu kwa Njia ya Nyimbo

Hizi hapa nyimbo mbili za Bahati Bukuku na tatu za Mchungaji Emmanuel Ushindi kutoka Bukavu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waimbaji hawa wanafanana katika uimbaji wao maana wote wanapenda kusimulia visa na mikasa katika nyimbo zao. Basi na ukaburudike na kujishibisha kiroho wakati unasikiliza nyimbo hizi za kupendeza !!!

Kama hutaki kuangalia video, au kama unataka kuzisikiliza nyimbo hizi kwa pamoja, bonyeza hapo kwenye audio chini ya post hii....

Bahati Bukuku

(1)  Mzee Tupa Tupa 


(2) Dunia Haina Huruma


Mch. Emmanuel Ushindi

(1) Bwana Nimeshindwa

(2) Hadithi Njoo


(3) Dunda Mu Yesu


Audio ya Nyimbo Zote Tano Hapo Juu Hii Hapa...

Sunday, March 10, 2013

Dunia Haina Huruma - Bahati Bukuku

Mkasa wa kusikitisha kuhusu jamii inayotaliwa na mfumo dume...
Kwa Mungu hata hivyo kila kitu chawezekana...

Tuesday, December 20, 2011

Bahati Bukuku: Sifai Kuwa Mke !!!



Na Brighton Masalu


MWIMBA Injili mwenye  muonekano wa ‘mama mwenye nyumba’  aliye pia na sauti ya uponyaji, Bahati Lusako Bukuku amefunguka akisema hafai kuwa mke na wala hafikirii kuolewa, paparazi wetu amebugia sentensi zenye ushahidi.


Bukuku aliyasema hayo mwanzoni mwa wiki hii alipokuwa akianika mwanya mbele ya ‘balozi’  wetu baada ya kumnasa shambani kwake, Bunju A Tegeta, jijini Dar es Salaam


Alisema miongoni mwa wanawake walioumbwa kwa ajili ya kuishi bila ndoa ni yeye na ndiyo maana alitimka kwa mumewe, Daniel Basila.


Aidha, alisema mwanaume huyo ni jasiri kwa sababu alimvumilia kwa vimbwanga na vituko vingi alivyokuwa akimfanyia ndani ya nyumba.Staa huyo wa wimbo wa Waraka, alizidi kukwea na mistari kuwa, Basila alidhani amepata mke bora kumbe alikosea uchaguzi jambo alilolifananisha na kuchukua mbavu za mbuzi kuzipeleka kwa tembo!


“Unajua jambo likikushinda huwezi kulazimisha, mimi nilidhani nafaa kuwa mke kumbe si kweli. Kifupi ni kwamba mimi kama Bahati Bukuku, sifai kuwa mke vinginevyo ni kumpa mwanaume stress (mawazo) zisizo na maana,” alitiririka Bukuku.


Pamoja na hayo, Risasi Jumamosi likaendelea kumchimba ili kutoka na ‘kavareji’ iliyoshiba kwa kumhoji kama kwa sasa anafikiria kuingia tena katika ndoa; 

Bukuku: Kama nilivyosema hapo awali hutakiwi kulazimisha jambo ambalo huliwezi, mimi suala la ndoa jamani siliwezi.


Risasi Jumamosi: Kwa hiyo ni kama una nuksi?


Bukuku: Hapana, siamini katika hilo, wala sijutii maana ni mipango ya Mola.


Risasi Jumamosi: Wewe ni mtumishi wa Mungu, kwake hakuna kinachoshindikana, sasa kwa nini usimuombe  akubadilishe na kukupa mume bora na mwema?


Bukuku: (akilikazia macho gazeti hili) mume bora nilipewa lakini yeye aliangukia kwa wrong person (mtu ambaye siye). Sasa labda kuna ambaye amempanga yeye, lakini nadhani nitaishi peke yangu hadi mwisho.


Risasi Jumamosi: Sasa jamii inakuchukuliaje? Kwani mwonekano na huduma unayoitoa unastahili kuwa na mume, maana wakati mwingine utahitajika kutoa ushauri kwa wanandoa ikiwa kama mtumishi.


Bukuku: (Kwa macho ya aibu) Duh! Labda husomi vizuri Biblia, maana ndoa inaruhusiwa kuvunjika na mimi niliwahi kuolewa na hata jamii inajua hilo. Ukweli ni kwamba siwezi kumhudumia mume ipasavyo.


Risasi Jumamosi: (likiongeza umakini zaidi) kwa nini?


Bukuku: Mfano, mume anakwambia mwende beach (ufukweni) na mimi nabeba khanga na gauni refu au wakati mwingine nakaa chumbani na mume wangu nikiwa nimevaa kimama zaidi, si nitamkera? Kifupi siwezi kuishi na mwanaume hasa kwa sasa, maana  kama ni ng’ombe, ameshazeeka.


Bahati Bukuku aliwahi kuolewa na Daniel Basila na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006.


Chanzo: Risasi