Kwa tunaoamini kwamba Biblia ni neno la Mungu, ni sawa kweli kuibadilishabadilisha mara kwa mara ili lugha yake iendane na wakati uliopo na mazingira tuliyomo?
Swali hili limezuka baada ya wafasri wa toleo jipya la mwaka huu la Biblia inayopendwa sana ya New International Version Bible (NIV) kuamua kutumia lugha inayoakisi usawa wa kijinsia. Kwa mfano, badala ya kusema, "If anyone says, 'I love God,' yet hates his brother, he is a liar.", sasa Biblia hiyo inasomeka "If anyone says, "I love God,' yet hates his brother or sister, he is a liar."
Kuna wanaodai kwamba Biblia ni neno la Mungu na kamwe haipaswi kuwa inabadilishwabadilishwa kila mara mikondo au matapo ya mawazo yanapobadilika katika jamii kwani kwa kufanya hivyo itafikia mahali tutakuwa tunapotosha kabisa maana iliyokusudiwa. Wewe unasemaje kuhusu suala hili?