Mchungaji Dr. Heri Muhando namfahamu na nilishawahi kuhudhuria mahubiri yake zamani. Ni mhubiri mwenye kipaji na mwenye bashasha na kidogo nimeshangazwa na taarifa hizi. Mafundisho ya utajirisho ni mazuri kama yakitumiwa vizuri kwani yanawapa watu nguvu mpya na matumaini kuyakabili maisha. Yasipotumiwa vizuri, hata hivyo, yanaifanya dini kuwa kama biashara tu kwani yanageuza mibaraka ya Mungu kuwa kitu kinachouzika na kununulika.
Hapa Marekani kwa mfano ni vurugu tupu na huwezi kujua kama kweli yanayotendeka ni kwa mapenzi ya Mungu ama la. Kuna wahubiri kila siku kwenye runinga wanaouza maji ya mibaraka, vitambaa vya miujiza na vipande vya mikate ambavyo wanadai kama ukikipata basi Mungu atafungua milango yake na utabarikiwa kimiujiza. Na watu hawa wana mashahidi lukuki ambao huelezea kwa kina jinsi walivyopata pesa nyingi bila kutegemea baada ya kununua vitu hivi. Mchungaji mwingine yeye huwataka watu "wapande mbegu" ya dola 1,000 tu halafu wataona mibaraka ya Mungu. Tena husisitiza kwamba hata kama huna basi ni lazima uende benki ukachukue mkopo umtumie hiyo "mbegu" ya dola 1,000 halafu ukae usubiri mavuno.
Kinachotia wasiwasi ni kwamba watu hawa wanaishi maisha ya kifahari sana mpaka mwaka huu baraza la Congress liliamua kuchunguza matumizi ya pesa zao kwani huwa hazilipiwi kodi. Ilibainika kwa mfano kwamba mchungaji mmoja alikuwa ametumia dola 25,000 (dola elfu 25!) kununulia choo (ile sehemu tu ya kukalia) na wengine walikuwa wametumia mamilioni ya dola kujinunulia ndege binafsi, magari ya kifahari, majumba na kufunga safari na familia zao kwenda kwenye mahoteli ya kifahari n.k. Hii kidogo mimi hunitatanisha. Wengine mna maoni gani kuhusu hii injili ya utajirisho?
Picha za gazeti la majira ni kutoka blogu ya Kennedy
12 comments:
Tunaishi siku za mwisho na yote yanayotokea sasa yametabiriwa katika Biblia. Wahubiri wengi hawa wanatafuta pesa tu na dini sasa ni njia ya mkato ya kujitajirisha. Wanawaindocrinate watu na kuwafanya watoe kila kitu na kubakia masikini wakati wenyewe wakiishi maisha ya kitajiri kupindukia. Nakupa miaka mitatu na utakuta huyu Mhando ni milionea wa dola na siyo madafu. Amewakimbia Wasabato wenzake kwa sababu walikuwa wanambana tu. Shika sana ulichonacho ili mtu mwingine asije akaichukua talanta yako!
Hizi ni siku za mwisho na lolote linawezekana. Mhando ni very good preacher na kama ni kutajirika basi atatajirika upesi hata kumzidi Kakobe. Kazi ipo!
Bwana Yesu asifiwe!
Mhando kwa kweli amewafanyia kituko cha ajabu wasabato. Nakumbuka katika mahubiri ya kisabato yaliyokuwa yanaendeshwa kwa fedha nyingi, mamilioni/mabilioni, ni mahubiri yaliyokuwa yakiendeshwa na Mhando. Watu walikuwa tayari kuuza baiskeli ili kazi ya Mungu iende mbele. Alikuwa akisimama hata kama una mia mbili ya nauli unaitoa. Nadhani huo moto katoka nao huko Marekani kama unavyoeleza ndugu yangu Matondo.
Sasa hii ni hatari kubwa.
Napenda nipingane kidogo na hawa wachangiaji wengine. Kanisa la Mungu huwa halichezewi. Mara nyingi Mungu amekuwa akilitetea sana kanisa lake. Alichofanya Mhando ni usaliti mkubwa mno. Na awe mwangalifu. Mungu katika historia amekuwa akiwashughulikia watu wake kikamilifu. Anaweza akalirudia kanisa la Mungu bila kupenda au akawa na experience tofauti na Kakobe na wengineo. Mungu hawezi kuruhusu ibilisi ajiinue, Atamshughulikia mpaka watu wamjue Mungu ni nani.
Mhando amefungua kanisa lake kwa majivuno makubwa sana. Huku akiwa anajua nuru ndogo inasemaje, amemkufuru Roho Mtakatifu. Shrti yake hadi atubu. Ole!
Aisee, ningekuwa Tanzania ningekimbia nikajiunge na hili kanisa jipya la Mhando kwani hapo kuna kutajirika haraka haraka tu...Kwa kweli hizi ni siku za mwisho!
Jamani mimi nimeamua kuanzia tarehe 1/1/2009 onwards sitatoa sadaka wala zaka kanisani hata senti tano.Sadaka yangu nitawapa masikini tena wale ninaowaona hawajiwezi kabisa yaani hawana mikono ya kufanya kazi au wana ulemavu unaowafanya washindwe kufanya kazi au wagonjwa.Wachungaji wanatuchanganya sana na maubiri yao,mara nyingine huwa nafikiri ni bora nikajifungia chumbani kwangu nikapiga magoti na kusali kuliko kwenda kanisani kuombwa hela.
Mdau wa January 3, 2009 2:21 PM umegonga kwenye pointi kabisa. Mimi nadhani kusaidia masikini moja kwa moja ni bora kuliko kuwapa hela za kutanulia hawa jamaa. Ukitoa kwa moyo mweupe moja kwa moja ni bora zaidi kuliko watu hawa ambao kusema kweli ni mafisadi wa kiroho. Ndiyo maana mimi simtegemei mchungaji kwa wokovu wangu kwani kwa hakika siku ya mwisho kitakuwa kilio na kusaga meno!
We anonymous wa January 1, 2009 4:29 PM. Mbona Padri Nkwera bado anapeta tu mbali na kutengwa na kanisa karibu miongo mitatu sasa? Kama Mhando amekimbia kwa sababu ya ufisadi na ubinafsi kanisani basi hakuna baya alilofanya ingawa hiyo injili yake ya utajirisho anayoikimbilia inatia shaka kidogo. Watu wengi waliowahi kufanya kazi katika taasisi za Wasabato kama mashule wamesikitishwa na ufisadi na ubinafsi uliotawala huko. Kanisa hili linalojidai kwamba eti ndilo la kweli inabidi lijisafishe na pengine hatua ya Mhando ni nzuri kama itaweza kuwaamsha watu. Mwacheni roho mtakatifu afanye kazi yake!
Lakini bwana wakubwa wa SDA wanapaswa kubadilika nao. Hivi ni kwa nini wasikubali watu waliokuwa wana mibaraka ya uponyaji huko kanisani kwao? Wao kama Mungu hajapitia kwao basi FULL STOP???!!!!!!!! Hii siyo poa kwa Mungu. Hata wafanyakazi wa huko Njiro wamegawanyika kwa imani ya ndani. Mhando ahubiri mambo ya utajirisho pekee mimi nimeishapokea mahubiri yake. Nimehudhuria mara mbili. Kwa kweli kuna mabadiliko kabisa na SDA ninayoijua ya huku bongo.
Wasabato madhehebu yote wanajua kuwa home ni MOTOOO. wabadilike
Njooni kwa YESU huku
Nakubaliana na mdau wa January 6, 2009 9:00 AM. Kuna wengi waliwahi kung'oka huko na bado wanamtumikia Mungu. Hata mie nawajua watu kibao tu walioanza kung'oka kabla ya Mhando. labda wataungana na Mhando.
Mhando ameona taa ila hata sie wa dhehebu zingine tusiache kumjenga huyu kondoo (mhando) ili asiendekeze ubinafsi kama huko alikoikong'oli quit.
There is nothing wrong kwa mkristo kuwa tajiri, Ibrahim, Sulemani, Yakobo, mfalme Daudi, Yusufu, hawa wote ni baadhi tu ya wachamungu ambao walikuwa matajiri, kwasasa tungewaita mamilionea, unamkumbuka Ayubu? so what am trying to say is... mafundisho yake kuhusu kutajirika kwa sasa tunayaona ni mapya kwa sababu it is not our culture kwetu sisi kam wasabato.
Biblia inasema usipotoa zaka umemuibia MUNGU, na pia inatuambia tumjaribu Mungu kwa sadaka na zaka tuone kama hatutafungukiwa madirsha ya mbinguni. Muhando sio Yesu sisi kama wakristo tunapaswa tuwe waangalifu na makini katika kusoma mandiko. Kama mafundisho anayoyatoa yako kwenye Biblia kwanini tunaogopa kumjaribu Mungu. Siri ya mafaninio ni moja kwa wale wanao amini Biblia. Toa zaka yako kamili.Kwa wasio elewa zaka ni nini kwa kifupi ni 10% ya mapato unayoyapata. Tusome maandiko na chamuhimu ni kufwata Yesu anasema nini. GOD bless you all.
Mrs tajiel Nyachia,
Bwana apewe sifa,Injili ya utajirisho ni upagani maana shetani anatumia njia hiyo kwa ajili ya kuteka watu wa Mungu.
Jamani tuache tabia ya kupenda pesa tutaangamia.
Bwana yesu Kristo Asifiwe sana.
Hakuna ubaya kwa Mkristo kuwa tajiri, Swali ni kwamaba, Alipataje utajiri? Je, anawanyang'anya watu pesa kwa Jina la Yesu? Anauza Muujiza wa Yesu ambao Yesu Alitupa bure? Nawe mkristo unaye toa je unasoma maandiko? Au unakubali kulaghaiwa na wanaotumia vibaya jina La Yesu? Mungu atubariki sana Lakini, tujue tunaishi nyakati za mwisho. Tuwe tayari kwa safari ya milele, Sasa, usiende ukauza ulichonacho ati unajiandaa, TAfadhali, ANDAA ROHO YAKO TU! NDIYO YESU ANA HAJA NAYO KWA AJILI YA PUMZIKO NA RAHA YA MILELE. Amen.
Post a Comment