Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Tuesday, December 30, 2008

MANABII WA UONGO - MCHUNGAJI MUNISHI

BREAKING NEWS: MCHUNGAJI MUHANDO ALIHAMA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

Mchungaji Dr. Heri Muhando namfahamu na nilishawahi kuhudhuria mahubiri yake zamani. Ni mhubiri mwenye kipaji na mwenye bashasha na kidogo nimeshangazwa na taarifa hizi. Mafundisho ya utajirisho ni mazuri kama yakitumiwa vizuri kwani yanawapa watu nguvu mpya na matumaini kuyakabili maisha. Yasipotumiwa vizuri, hata hivyo, yanaifanya dini kuwa kama biashara tu kwani yanageuza mibaraka ya Mungu kuwa kitu kinachouzika na kununulika. 

Hapa Marekani kwa mfano ni vurugu tupu na huwezi kujua kama kweli yanayotendeka ni kwa mapenzi ya Mungu ama la. Kuna wahubiri kila siku kwenye runinga wanaouza maji ya mibaraka, vitambaa vya miujiza na vipande vya mikate ambavyo wanadai kama ukikipata basi Mungu atafungua milango yake na utabarikiwa kimiujiza. Na watu hawa wana mashahidi lukuki ambao huelezea kwa kina jinsi walivyopata pesa nyingi bila kutegemea baada ya kununua vitu hivi. Mchungaji mwingine yeye huwataka watu "wapande mbegu" ya dola 1,000 tu halafu wataona mibaraka ya Mungu. Tena husisitiza kwamba hata kama huna basi ni lazima uende benki ukachukue mkopo umtumie hiyo "mbegu" ya dola 1,000 halafu ukae usubiri mavuno. 

Kinachotia wasiwasi ni kwamba watu hawa wanaishi maisha ya kifahari sana mpaka mwaka huu baraza la Congress liliamua kuchunguza matumizi ya pesa zao kwani huwa hazilipiwi kodi. Ilibainika kwa mfano kwamba mchungaji mmoja alikuwa ametumia dola 25,000 (dola elfu 25!) kununulia choo (ile sehemu tu ya kukalia) na wengine walikuwa wametumia mamilioni ya dola kujinunulia ndege binafsi, magari ya kifahari, majumba na kufunga safari na familia zao kwenda kwenye mahoteli ya kifahari n.k. Hii kidogo mimi hunitatanisha. Wengine mna maoni gani kuhusu hii injili ya utajirisho?

























Picha za gazeti la majira ni kutoka blogu ya Kennedy

NJIA PANDA - NEEMA MUSHI NA KWAYA YA NEW LIFE CRUSADE (TABATA)

MAMA AKAITIKA - KWAYA YA MTAKATIFU CECILIA ARUSHA

KUTANIKENI - KWAYA YA A.I.C MAKONGORO

KANDO YA MITO - KWAYA YA MAMAJUSI MOSHI

NIKUPE NINI - KWAYA YA ST. JOSEPH MIGORI

ONJENI - ROSE MUHANDO