MAHUBIRI YA MZEE WA UPAKO NA MTUME/NABII JOSEPHAT MWINGIRA

Mahubiri ya Mzee wa Upako

Mahubiri ya Mtume na Nabii Josephat Mwingira

Saturday, June 20, 2009

NIBEBE - ROSE MUHANDO

10 comments:

Anonymous said...

Wimbo mzuri sana huu. Nilipomwona huyo kijana Zeruzeru nimekumbuka jinsi binadamu tulivyofikia mbali na kuanza kuuana kwa sababu za ajabu ajabu. Shetani ni kweli ametawala hapa duniani. Tushike sana tulichonacho. Dada Rose, endeleza injili. Nimelia sana na nimeguswa - tena kwa namna ambayo sijawahi hata nikiwa kanisani. Na Prof. uliyeweka hizi nyimbo hapa ubarikiwe pia. Umeacha kiburi cha elimu na kuamua kumtumikia Mungu. Mungu atubariki sote tukaze mwendo na tumwite Yesu aje atubebe!

Anonymous said...

Huyo kijana kilema amenifanya nilengwelengwe na machozi. Kazi nzuri sana dada Rose

Anonymous said...

Rose you have been a blessing to my soul and especially the lame man who has made me look at myself with both hands and legs to praise my saviour more. Let God atubebe in this sinful time. Thanks sister Rose. How can i get all your vidoes that you have produced?
I live in Minnesota USA

Anonymous said...

Rose Wewe Mungu aliye Juu Akubariki kwa ajili ya kazi hii nzuri ya kueneza Injili yake Hapa Duniani.Bwana Akubariki sana Dada Rose Nimependezwa na Nyimbo hizi na kuguswa na Mguso mpya nikiwa hapa Marekani.
Raphael Gathuru.

Mzee wa Changamoto said...

Wow! Kweli watu huzaliwa kufanya kitu. Wimbo huu ni zaidi ya ubalozi wa nini kinaimbwa. Unagusa kusikiliza, unagusa kuangalia na kwa hakika ni kazi nzuri.
Naungana na walioanguliwa kuwa ni kati ya kazi nzuri saana za kisanii kumuimbia Mungu.
Baraka kwako Da Rose nawe Prof.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mzee wa Changamoto;
Ndiyo, Rose Mhando ni msanii aliyekomaa na kwa maoni yangu ndiye msanii bora kabisa katika nyimbo za Injili za Kiswahili. Unajua nilifikiria siku moja kuhusu jambo hili baada ya kuona muda ambao nautumia katika mtandao kusoma habari za CNN, Michuzi n.k. Nikaona kwamba wakati nasoma hizi habari naweza pia kuwa napandisha nyimbo za dini. Nikajaribu nikaona si vigumu na naona nimepiga hatua. Nyimbo hizi zimetapakaa kila mahali mtandaoni na kuziweka pamoja namna hii naamini lilikuwa wazo zuri na nitaendelea kufanya hivyo. Asante!

Yasinta Ngonyani said...

Wimbo huu nausikiliza kila jpili naopenda sana yaani basi tu na dada Rose amebarikiwa kuwa na sauti nzuri. Leo nimemsikiliza kwenye BBC jinsi alivyopitia maisha yake. Ubarikiwe sana dada Rose

mwamyinga said...

Dada Rose ,wimbo wako huu ni mzuri kupita kiasi na una ujumbe murua.Lakini naomba niwe muwazi kwa kusema kwamba ule wimbo wako wa MOYO WANGU ndio naupenda kupita maelezo haya nilioandika hapa. Ubarikiwe sana Mungu azidi kukupa nguvu na afya njema ili uzidi kuendeleza Injili kwa njia ya nyimbo.

mechaque said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Rose Muhando is a light in east africa. she sings wholeheartedly and with vigor and might. Her songs are full of teachings. Thank you Rosie