- Sinema ya Maisha ya Yesu sasa inapatikana mtandoni katika lugha mbalimbali za Kitanzania kama Kibena, Kidigo, Kigogo, Kihaya, Kihehe, Kimasai, Kimeru, Kimoshi (Kichaga), Kimakonde, Kimakua, Kinyakyusa, Kinyilamba, Kimasai, Kinyamwezi, Kinyakyusa (cha Ngonde), Kishambala, Kisukuma, Kiswahili na Kiyao.
- Sinema hii pia inapatikana katika lugha nyingine za Afrika. Ukitaka kuisikiliza na kuitazama, tembelea tovuti ifuatayo na chagua lugha unayotaka.
- Pia unaweza kusoma Biblia, kusikiliza na kutazama filamu ya Yesu pamoja na rekodi mbalimbali za Kikristo katika lugha kadhaa za Tanzania kupitia tovuti ya Joshua Project (chagua Tanzania). Mungu Atubariki tunapouanza mwaka mpya wa 2011.
No comments:
Post a Comment