MAHUBIRI YA MZEE WA UPAKO NA MTUME/NABII JOSEPHAT MWINGIRA

Mahubiri ya Mzee wa Upako

Mahubiri ya Mtume na Nabii Josephat Mwingira

Sunday, December 19, 2010

YESU KRISTO - MFALME WA FALSAFA?

Nawasalimuni wote ndugu zangu. Naomba nirejee tena na mada hii ambayo imenipa kufikiri sana bila kupata muafaka wa mawazo yangu. Nimejihisi kuwa labda nimekuwa mvivu wa kusoma maandiko matakatifu ya Mungu.

Yesu anatajwa sana habari zake na hivi karibuni tunaelekea kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwake. Pamoja na jitihada zote za kutaka kufahamu kwa nini Yesu alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kujibu maswali yote aliyoulizwa, nimekosa habari zake muhimu.
  • Yesu mnazareti, aliyezaliwa na Bikira Mariam, alisoma shule gani na chuo kipi?
  • Naomba kujua kiwango chake cha elimu.
Makuhani, Maliwali, Mafarisayo na wasomi wengine waliuliza maswali mengi kutaka kumtega, lakini Yesu alikuwa na uwezo wa kutoa hadi "reference" kwa kusema " IMEANDIKWA". Hata nyoka alipotaka kumjaribu Yesu, alijibu "IMEANDIKWA usimjaribu Bwana Mungu wako"
  • Kwa nini walimwita Mwalimu hata wasomi waliokuwa na elimu ya juu katika Uyahudi?

"NAWATAKIA CHISTMAS NJEMA NA HERI YA MWAKA MPYA 2011"


Maswali haya yako hapa

4 comments:

Amos Msengi said...

Nashukuru sana Matondo kwa kuliwezesha swali hili, sijapata majibu, huyu jamaa Yesu alikuwa na elimu ambayo haijawahi kuwako hadi leo. Maranyingi tumeita kila jambo alilofanya Yesu kuwa ni miujiza, lakini naona vyema tusiwahi kusema hivyo, tuangalie elimu aliyokuwanayo ni ya kiwango cha juu, kuna miujiza ndio sikatai, kabla ya kuhitimisha hilo tujiulize leo hii hata nasi twajua mengi ambayo enzi za Yesu tulikuwa hatujui. Nahisi taratibu tutafikia kiwango chake miaka ijayo.

Anonymous said...

Wacha wee! Hongera sana kaka. Soma sana tu, pengine miaka ijayo utafikia "kiwango cha Yesu" kama ulivyosema!

Ila nna mashaka kidogo!!! Natania tu!

Anonymous said...

EV.MGENI,T seoul Korea.
Ndugu uliyeuliza swali ningependa kukupongeza kwa kuwa roho wa mungu amekufunulia kuwa hakuna elimu, maarifa au elimu ya kweli itokayo kwa wanadamu. Kwa kifupi Yesu hakusoma elimu yoyote ya duniani. Ikumbukwe kuwa neno la mungu linasema kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa,Mith1:7 hivyo ufahamu wa Yesu ulitokana na Roho wa mungu awezaye kuleta maarifa ya hali ya juu ukilinganisha na ya wanadamu. Hii ndiyo maana wasomi wa nyakati za yesu kama Nikodemo na baadaye akina Sauli/Paulo walitambua kuwa elimu yao ni bure kama mtu hakutembea ktk Roho. Fikiri kuhusu Yusufu aliyekuwa na uwezo kushinda wasomi na wajuzi wote wa misri bila darasa.mw.41:38-40 au Daniel licha ya kwenda shule aliongezewa uwezo wa ufahamu mara kumi zaidi kuliko wakalidayo wasiyomjua mungu.Dan.1:17-20.
na kuna mifano mingine mingi tu ktk biblia hata wewe unaweza kufikia kiwango cha Yesu ukiamua kumaanisha katika kumcha Mungu.

Arrah said...

Asante sana Anony wa pili kwa mchango wako mzuri ambao ume base katika Agano la Kale. Na hata katika Agano Jipya kuna mengi sana ya kujifunza kuhusu uweza wa Yesu, na Ahadi zake kwao wamwaminio ("UKIAMINI UTAWEZA KUFANYA HATA ZAIDI YA HAYA" -aliyoyafanya Yesu). Ila kaka Msengi sijui uliposema "kusoma" ulimaanisha elimu ipi..? Otherwise, huwa kuna kiji-mgongano kidogo kati ya "elimu-dunia" hasa uki base katika mambo ya Kisayansi na elimu ya Mungu, ambayo kwa SEHEMU KUBWA (note that) ina base katika IMANI! Kuna scholars wengi waliojaribu ku harmonise sayansi na imani (nitakutajia wachache ujaribu kufuatilia mawazo yao), na hata ku question God's incarnation (kuzaliwa kwa Yesu kwa kupitia bikira Maria), na mambo mengine mengi ambayo Kisayansi unaishia hewani! Kwa hiyo, kama Anony 2 alivyochanganua (na mimi pengine kuna siku nitatoa maoni yangu), unaposema "utasoma na kufikia kiwango cha Yesu", kwangu mimi naona itategemea unasoma kwa "kuegemea upande gani!" Duh! Sidhani kama nna maneno ya "Kuelezea kilicho katika mind yangu!" Nitaeleza vizuri siku nyingine.
Stay blessed!