- Wapendwa; nilikuwa sijui kwamba tayari tumeshagonga watembeleaji zaidi ya milioni moja. Mibaraka iliyoje! Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuruni nyote kwa ushirikiano wenu ambao umeifanya blogu hii ifike hapa ilipo.
- Lengo langu pekee la kuanzisha blogu hii ilikuwa ni kuzikusanya nyimbo za injili zilizotapakaa mtandaoni katika sehemu moja. Wapo waliokerwa na jambo hili na wengine wakafikia hata kuomba nyimbo zao ziondolewe hapa kwani zilikuwa zinawaharibia biashara. Lengo langu kamwe halikuwa kujipatia fedha na sijapata hata senti moja kupitia blogu hii. Ndiyo maana hakuna matangazo ya aina yo yote ile katika blogu hii pamoja na ukweli kwamba huwa napata maombi ya watu na makampuni mbalimbali kutoka Tanzania wakitaka kuweka matangazo yao hapo juu ya blogu kwa malipo.
- Kama kuna mtu hata mmoja tu ambaye aliweza kuguswa na nyimbo zilizopo hapa kiasi cha kurudisha ukaribu wake na Mungu wetu, basi lengo langu la kuanzisha hii blogu litakuwa limefanikiwa. Kwa moyo mkunjufu napenda kuwashukuruni nyote. Na kwa wote waliokwaza kwa namna yo yote ile, samahani sana. Na mlango uko wazi. Kama unataka nyimbo fulani tuziondoe hapa basi usisite kutujulisha nasi tutafanya hivyo mara moja - hata kama ni kuifunga blogu hii. Mungu hategemei kiblogu kama kama hiki ili kufikisha ujumbe wake kwa watu Anaowatafuta. Kwake hata mawe yaweza kupiga kelele na kuutangaza ufalme wake ujao!
- Kama una maoni yo yote kuhusu jinsi ya kuiboresha na kuiendeleza blogu hii basi usisite kutujulisha. Tatizo kubwa ni kwamba mimi mwenyewe si mtaalamu sana wa haya mambo ya kompyuta na huwa nasonga mbele hivyo hivyo tu kwa kubangaiza. Mungu daima ni Mwema ati!
Asanteni sana na Mungu Aendelee kutubariki !!!
6 comments:
Mwanadamu hata kamwe hatampendeza mwanadamu mwenzake kwa jambo lolotemia kwa mia,
Nakushukuru sana kwa bidii unayo kwa kazi hii,nabarikiwa sana na nyimbo hata mahubiri.
Hallo Amani,
Kwanza namshukuru Mungu aliyekupa kipaji kizuri sana cha kukitumia kukusanya nyimbo zote hizo kitaalamu kabisa.
Mimi ni mmojawapo wa watu wako ambao wanatumia blog hii kama chakula chao cha kila siku.Nasikiliza nyimbo za humu blogini kuanzia saa 12-6 usiku kila siku. Nimebarikiwa sana na wakati mwingine nikiwa ofisini basi nawekeza taratibu ili wazungu wasiudhike na makele.Kwa namna nyingine umenisaidia sana huku ughaibuni ukiwa unaondoka na Neno la Mungu nalipa vema kupitia nyimbo hizo.
Amani, nakuombea uzidi kukusanya hizo nyimbo naamini wokovu utapatikana kwa wengi kupitia kazi yako njema sana.Ubarikiwe sana na Mungu azidi kukutia nguvu katika hilo.
Katika blog zote ni blog yako tu naipa heshima sana maana nimebarikiwa nayo sana hasa katika kupata chakula cha kiroho kupitia nyimbo za watumishi mbalimbali.
Mungu ni mwema sana aliyekupa mawazo maelekevu kufikiri kufanya jambo jema namna hiyo.Nisipotembelea hapa blogini basi siku hiyo niko safarini.
Mimi nashukuru sana kwa Blog hii!naiendelee mbele zaidi!kwani nafarijika sana na napata nyimbo nyingine za zamani sikujua wapi nitapata!
Mungu awabariki na kuwatia nguvu!
pamija katika yote yampendezayo Mungu!.Amen.
Binafsi ninamshukuru Mungu sana kwa ajili ya kukupa uwezo na ubunifu mkubwa sana wa kuanzisha blog hii.
Nakumbuka siku ya kwanza kuingia ktk blog hii kwa kweli sikuelekezwa na mtu ila nilikuwa nimechoka sana nikawa najaribu kuandika baadhi ya maneno kwenye internet ili kupata mahubiri basi kwa neema ya Mungu nikajikuta nipo ktk blog hii. Nakumbuka nilisikiliza mahubiri yale, yalikuwa ya Mtumishi wa Mungu Mwakasege nilipata faraja ya pekee na nguvu mpya.
Mpendwa kazi yako sio bure ktk Kristo, fanya kwa bidii wako wengi tuliokutana na mahitaji yetu kupitia ktk blog hii.Mungu akubariki.
Asanteni sana ndugu zangu. Inanipa moyo na kunifariji mno kuona kwamba kumbe kazi yangu ya kuzikusanya video na nyimbo za injili katika Blogu hii si bure!
Asanteni sana na Mungu Aendelee kutubariki. Japo niko "busy" na mambo mbalimbali ya kidunia, blogu hii ilikuwa/ni njia mojawapo ya kuitikia wito wa Bwana wa "Nendeni Mkaieneze Injili kwa mataifa yote" Sote hatuwezi kuwa wachungaji. Hebu basi kila mmoja wetu na akaweze kufanya kile awezacho katika kuhakikisha kwamba Injili inasonga mbele! Usisubiri mpaka wakati utakapokuwa na muda. Ati, wajuaje kama utakuwa na muda????
Safari ni lazima iendelee ati!
Post a Comment