Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Lengo kuu la blogu ya nyimbozadini ni kuzikusanya video na audio mbalimbali za nyimbo za dini na kuziweka pamoja. Tunatumaini kwamba hii itawapunguzia shida ya kuhangaika kwenda katika mitandao mbalimbali kusaka video na audio hizi. Kwa hivyo video na nyimbo zote zilizopo hapa zinapatikana mtandaoni katika tovuti mbalimbali kama Youtube.com na Google videos. Nyimbozadini.Blogspot.Com haitunzi wala kuuza nyimbo zo zote na kama unataka kununua video za nyimbo utakazoziona hapa basi wasiliana na watoaji au wamiliki wa video hizo. Karibuni tuburudishe mioyo, roho na fikra zetu kwa nyimbo motomoto za Injili. Mungu Atubariki sana!!!
3 comments:
Wimbo mzuri sana lakini huyo jamaa wa pili kauharibu. Sijui kwa nini walimwachia aharibu vile. Pengine ni mtoto wa mchungaji au mwenyekiti wa kwaya...
Ujumbe mwema sana. Ila nimepata taabu kutambua ni aina gani ya muziki huyo jamaa wa pili alitaka kuitumia. Ni kama R&B ambayo anaimba juu ya mapigo yasiyo yake. Kwa hakika ameharibu na kama wanaweza kuurejea na kurekebisha hapo basi ujumbe utafika zaidi. Kwa sasa nimeshajua pa kukatisha nikiwa nasikiliza (maana sitaki kukwazika)
Huyo jamaa wa pili ni mwanakwaya au wamemwokota tu barabarani na kumwambia twende tukashuti video? Kauharibu wimbo wote nyang'anyang'a kabisa. Yaani inakuwa kama American Idol pale mwanzoni mwanzoni. Itabidi warudie hii video aisee. Au kama unaweza kui-edit fanya hivyo umtoe huyu jamaa wa pili
Post a Comment