Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Lengo kuu la blogu ya nyimbozadini ni kuzikusanya video na audio mbalimbali za nyimbo za dini na kuziweka pamoja. Tunatumaini kwamba hii itawapunguzia shida ya kuhangaika kwenda katika mitandao mbalimbali kusaka video na audio hizi. Kwa hivyo video na nyimbo zote zilizopo hapa zinapatikana mtandaoni katika tovuti mbalimbali kama Youtube.com na Google videos. Nyimbozadini.Blogspot.Com haitunzi wala kuuza nyimbo zo zote na kama unataka kununua video za nyimbo utakazoziona hapa basi wasiliana na watoaji au wamiliki wa video hizo. Karibuni tuburudishe mioyo, roho na fikra zetu kwa nyimbo motomoto za Injili. Mungu Atubariki sana!!!
3 comments:
Hey nice I liked the song,sasa I need your help,natafuta nyimbo zilizo imbwa na kwaya ya arusha mjini kama "ole wake umsaliti,kila mtu na mzigo wake etc niandikie jinsi yakuzipata online
Bwana Lema;
Mimi ninachofanya ni kukusanya hizi nyimbo kutoka tovuti mbalimbali mtandaoni na kuziweka hapa. Nyimbo karibu zote hapa zinapatikana katika youtube. Niliona kwamba ni vizuri zaidi kuziweka pamoja kuliko kwenda youtube na kuanza kusaka wimbo mmoja mmoja. Hizo nyimbo unazozitafuta jaribu ku-google na pengine kuna mtu tayari ambaye ameshaziweka mtandaoni.
Good to see Kenyan gospel on your site. Great stuff and keep it up!
Post a Comment