Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Lengo kuu la blogu ya nyimbozadini ni kuzikusanya video na audio mbalimbali za nyimbo za dini na kuziweka pamoja. Tunatumaini kwamba hii itawapunguzia shida ya kuhangaika kwenda katika mitandao mbalimbali kusaka video na audio hizi. Kwa hivyo video na nyimbo zote zilizopo hapa zinapatikana mtandaoni katika tovuti mbalimbali kama Youtube.com na Google videos. Nyimbozadini.Blogspot.Com haitunzi wala kuuza nyimbo zo zote na kama unataka kununua video za nyimbo utakazoziona hapa basi wasiliana na watoaji au wamiliki wa video hizo. Karibuni tuburudishe mioyo, roho na fikra zetu kwa nyimbo motomoto za Injili. Mungu Atubariki sana!!!
5 comments:
Hiyo picha ya kwanza ina suggest hii blog ni ya nyimbo za Kenya. Lakini blog imejaa nyimbo za Tanzania .
mwimbo mzuri nimeupenda. Kwani kusikiliza nyimbo si lazima ziwe kutoka TZ tu nyimbo ni nyimbo tu
We Anonymous. Kuna shida gani kusikiliza nyimbo za Kenya? Kama alivyosema Yasinta, hata mimi sielewi tatizo ni nini. Ni wimbo hukuupenda au nyimbo za dini za Kenya ndiyo tatizo? Huo ni wimbo na umetengenezwa na Kenyangospel.com. Tatizo liko wapi? Fafanua please!
OK, DADA NGONYANI. MWAFRIKAKUJIVUNIA KILIMANJARO SI TATIZO.
KUNA WA SENEGAL WANA CLUB WANAIITA KILIMANJARO.
HIYO NI TOFAUTI NA KUSEMA MT KILIMANJARO UPO KENYA.
IDENTITY VIOLATION NIMEIONA HATA KTK EASTAFRICAN TUBE.
Wewe usiye na jina hapo juu usichanganye watu hapa na mambo yako ya utaifa, ukabila na siasa. Nadhani unahitaji maombi wewe. Kama unataka mjadala wa haya mambo yako ya utaifa na ukabila nenda ukasome makala za Mobhare Matinyi katika IssaMichuzi.blogspot.com na kama unazo points basi ka-argue huko. Hapa si mahali pake na please tuache tupate injili bila kujali UTAIFA. Yesu mwenyewe alisema NENDENI MKAITANGAZE INJILI KATIKA MATAIFA YOTE...Hakusema mkifika Kenya fanyeni hivi, mkifika Tanzania fanyeni hivi...Ubarikiwe!
Post a Comment