Somo la 8: Kutimiza Unabii wa Agano la Kale
-
*Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu*
*(Yohana 2, 3, 5, 8 & 19)*
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2024, Bruce N. Cameron, J.D.
Kwa wana...
3 days ago
8 comments:
Acheni injili ya Mungu ihubiriwe popote pale. Kutakuwa na sherehe na vifijo mbinguni kama mlevi mmoja ataokolewa. Mimi nadhani ni sawa tu kupiga nyimbo za dini kwenye mabaa. Huwezi jua mipango ya Mungu.....
Mimi ni Mkristu. Sielewi kwa nini nyimbo za dini yetu zinapigwa kwenye baa. Wakristu tukiendekeza tabia hii ya kutopambanua masuala ya ibada na masuala ya ulabu, mwishoni tutakuwa tunatwanga bia kanisani.
Kuna masuala mengine ambayo yanaonyesha kuwa Wakristu tumepotea njia. Vitabu vyetu vitakatifu, kama Biblia, utavikuta vimezagaa hata gesti, katikati ya vyupa vya bia na konyagi na vitu vingine visivyotajika. Muislam namheshimu, kwani anaheshimu vitabu vya dini yake. Hutavikuta vimezagaa namna hiyo.
Hata hizo nyimbo za dini zinazotamba baa ni za dini yetu Wakristu. Sijamwona Muislamu akidhalilishi nyimbo za dini yake namna hii.
Mimi nadhani nitasilimu tu na kuwa Mwisilamu. Ninaamini kwamba Biblia yetu imechafaliwa sana kwa kutafsriwa hovyo hovyo. Leo hii Ukristo umegeuzwa biashara. Tazama akina Kakobe walivyojitajirisha kwa kutumia fungu la 10 kutoka kwa waumini waliokuwa "indocrinated" Inasikitisha sana! Biblia, nyimbo na kila kitu cha Kikristo unaweza kukifanya cho chote unachotaka. Hebu iguse Korani uone moto utakavyokuwakia!
Wapendwa, kuna mambo mengi ambayo yatakiwa kufanyiwa marekebisho, hasa kwa habari ya Ukristo. Tunasahau jina tulilonalo la kuitwa "Mkristo" kuwa ni jina la ajabu. Jambo lingine mara nyingi tumesahau habari ya Mungu wetu kuwa "Roho" nao wamwabuduo inawalazimu kumwabudu katika Roho.
Nadhani tukiyafahamu yayo, na kusudi letu kama Wakristo, nadhani tutaweza kuyatenda yatupasayo.
Mungu atusaidie wote tujue tu viungo katika mwili wa Kristo, zaidi sana kazi ya kila kiungo katika kuikamilisha.
Mmmmh! Mjadala mkubwa na mzuri huu. Kama nilivyowahi kusema, kuna mengine ya kujiuliza kuhusu maisha yetu. Bado nahisi kuna ukweli katika hili lililosemwa japo naamini kuna wanaolikuza kuliko lilivyo. Nimekuwa na mijadala kadhaa kule Strictly Gospel kuhusu hili na mengine mengi. Tatizo linakuja pale ambapo wenye kuonekana wanatetea, wanakuja na references ambazo zinaonesha mapungufu mengi ya uelewa wa Neno la Mungu. Lakini nami niliwahi kuuliza matumizi ya NENO LA MUNGU kwa dini zote kwa namna linavyotumiwa na viongozi mbalimbali. Bofya hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/hivi-marais-wana-dini-ama-imani.html kusaidia kuona kama tunatenda tusemalo ama tunasema kwa kuwa ni utaratibu na kutenda kwa kuwa sehemu ya maisha inatulazimisha kutenda hivyo. Wanaopiga nyimbo za injili, ni kwa kuwa zinaleta wateja, japo wanajua kuwa haziendani na "biashara" zao. Lakini unapokosa muungano wa Imani yako na Maisha yako ya nje, maisha hayatakuwa sawasawa.
Sasa na huyu Injilia kalitumiaje neno la Mungu? http://issamichuzi.blogspot.com/2009/06/aua-wawili-na-kujeruhi-saba-kwenye.html#comments
Ni sawa, Yesu hakuja kwa watu safi, bali waliopotea. Mtu mzima haitaji tabibu...
Waache wapate neno la Mungu hukohuko baa. Kila mtu alisikie neno kabla huo mwisho haujaja....
Ni hayo tuuuuuu
mtoa maoni anayesema utasirimu mimi nakushauri kuwa kubadili dini sio suluhisho kwani huko nako kuna matatizo makubwa inawezekana zaidi ya hayo mfano watu kujitoa muhanga na kuuwa watu wasio na hatia au kuwapiga wanawake wazinzi mawe hadi wanafariki dunia hivyo kabla hujafanya jambo jaribu kufikiria mara mbili mbili
Post a Comment