Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Lengo kuu la blogu ya nyimbozadini ni kuzikusanya video na audio mbalimbali za nyimbo za dini na kuziweka pamoja. Tunatumaini kwamba hii itawapunguzia shida ya kuhangaika kwenda katika mitandao mbalimbali kusaka video na audio hizi. Kwa hivyo video na nyimbo zote zilizopo hapa zinapatikana mtandaoni katika tovuti mbalimbali kama Youtube.com na Google videos. Nyimbozadini.Blogspot.Com haitunzi wala kuuza nyimbo zo zote na kama unataka kununua video za nyimbo utakazoziona hapa basi wasiliana na watoaji au wamiliki wa video hizo. Karibuni tuburudishe mioyo, roho na fikra zetu kwa nyimbo motomoto za Injili. Mungu Atubariki sana!!!
5 comments:
Rose Muhando wewe kweli ni kiboko. Nyimbo zako zinaburudisha, zinavutia, zinafanya mtu uwe karibu na Mungu wako na zaidi ya yote zinatia moyo sana. Mungu aendelee kukubariki ili uendelee kumtumikia zaidi.
Ni kweli kabisa nami nasema Mungu aazidi kukubariki ili wengine tuzidi kuburudika huu wimbo umekuwa kama sara ya baba yetu...
Rose, Mungu aendelee kukubariki dadangu. Mtumikie Mungu mpaka siku yako ya mwisho hapa duniani. Tena umenifurahisha sana kwa jinsi unavyojua kukata mauno...
Laiti mgejua Rose Muhando! msingesema hivyo, ni mfanyabiashara mzuri, maisha yake hayana ushuhuda kabisa! Mungu amekupa kipawa dada, lakini tumia kwa utukufu wake! We all love you!
We Joseph, kwani kufanya biashara ni vibaya? Unataka akale wapi? Tusiangalie mabaya tu. Dada huyu ametoa mchango mkubwa sana katika kukua kwa nyimbo za injili katika ulimwengu wa Kiswahili. Ubarikiwe Rose - usiwajali the haters!!!
Post a Comment