Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kisukuma
  
Audio ya Sinema ya Yesu Katika Kiswahili

Wednesday, March 31, 2010

SHUTUMA KALI KWA WAIMBA WA NYIMBO ZA INJILI - ETI WENGI WAO WATAENDA MOTONI

Waimbaji wengi wa muziki wa Injili watatupwa motoni


Ni siku nyingine imempendeza Mungu tukutane katika mtando huu kwa ajili ya kuangalia muziki wetu wa injili. 

Yawezekana wewe unaweza ukawa shahidi wa hili ninalolizungumza leo katika blog hii. Hakuna asiyetambua kwamba muziki wa injili kwa kiasi kikubwa umekuwa ukiwasaidia watu wengi waliokwenye dimbwi la kufanya maovu kuachana na tabia hiyo na kumrudia Muumba wao kwa kuokoka kutokana na maneno mazito na yenye ushawishi ambayo hutumiwa na muimbaji binafsi, kwaya ama kikundi.

Chakusikitisha katika hili ni kwamba, baadhi ya waimbaji wa muziki huo wameonekana kama kibao cha matangazo kinachomwelekeza mtu kwenda sehemu anayotaka kwenda kama haijui. Matangazo ama mabango mengi ya namna hiyo yamefanyika msaada mkubwa kwa kuwafikisha watu sehemu husika bila usumbufu huku menyewe yakibaki hapo mpaka wakati mwingine yanaota kutu.
 
Mbali na kuonekana kutoa msaada mkubwa kwa wahusika lakini bango mwisho wa siku hung’olewa na kwenda kutupwa jalalani baada ya kuchakaa na kuonekana uchafu sehemu husika. Leo hii baadhi ya waimbaji wa muziki wa Injili wamekuwa kama mabango ya kuelekeza watu kuachana maovu na mwisho wa siku kufika salama kwa Muumba wao huku wao wakibaki palepele.

Waimbaji hao asilimia kubwa wamekuwa wakifanya usanii wakati wa kuimba madhabauni kwa kuonekana wanaimba katika roho na kweli mpaka watu wanabarikiwa kutokana na kuimba kwa usitadi wa hali ya juu na sauti zilizopangiliwa vema.

Kama unafikiri na nakudanganya, jaribu kuchunguza kwa umakini, waimbaji wengi leo hii ni waasherati wakubwa, tena wanachukuana wao kwa wao ndani  ya kwaya na vikundi vyao. Utakuta wanakwaya wanafanya uchafu huo kwa siri kubwa na hao hao wanasimama kwenye madhabahu kuimba nyimbo za kukemea kuachana na maovu pasipo kuangalia kibanzi kilicho ndani ya macho yao

Ukifanikiwa kusikiliza nyimbo zao radioni ama kwenye luninga kwa waliofanikiwa kurekodi, utawaona wanaiba kwa kuhisia kali kana kwamba hata leo Masihi akiwachukua wanaenda moja kwa moja peponi, lakini ukweli ni kwamba huo ni usanii pekee na siku ya mwisho nafikiri ndiyo watakuwa wakwanza kutuwa motoni.

Mimi sielewi ni Mungu yupi wanaomtumika waimbaji wenye tabia hiyo chafu, kwa maana mbali na kufanya uasherati, watumishi hao hao ndiyo walevi, wasengenyaji, wadokozi, wambeya na wenye maneno machufu kinywani mwao.

Inauma sana unaposiki baadhi ya waimbaji wanaenda kwa  waganga wa kienyeji kwa lengo la kusafisha nyota zao ili nyimbo zao zipate kibali machoni mwa Watanzania na hata nje ya nchi. Bila aibu baadhi yao huwa wanafukiza dawa kabla ya kupanda madhabahuni ili anatakapopewa nafasi kuimba kila mmoja amfurahie na  ikiwa pamoja na kutuzwa fedha kutokana na uimbaji mzuri.

Sasa swali unaweza kujiuliza, inakuaje watu hawa wanatenda maovu na wanaimba kwa upako lakini Mungu bado amewaruhusu kufanya hivyo? Jibu ni kwamba kipindi hiki ni cha neema, Mungu anakuwa kama hawaoni, lakini ukweli ni kwamba ipo siku atakuja kuwafedhehesha saa na majira wasiyoyajua.

Hivi karibuni nilibahatika kuzungumza na muimbaji wa muziki wa Injili David Robert ambaye naye bila kicho alikiri kuwepo kwa tabia hiyo na kusema kuwamba hiyo inatokana na baadhi ya waimbaji kuendeleza  tabia zao waliokuwa nazo kabla ya kuokoka.

“Kaka kuokoka ni rahisi lakini kuutunza wokovu ni kazi kubwa, ndiyo maana waimbaji hao ambao huokoka baada ya kupanda neno la Mungu, wasiposimama imara hujikuta wanarudi nyuma kutokana na kukumbuka walikotoka,” alisema Robert


Nyimbozadini.blogspot.com tunasema: Sisi ni nani mpaka tuhukumu???  

    3 comments:

    Anonymous said...

    Jamani, Mungu haangalii kama binadamu aangaliavyo...wewe ni nani mpaka uwashutumu wenzako, hebu tafadhali badala ya kushutumu, waombee na Mungu atafanya lililo kweli

    Anonymous said...

    Anony - kweli tupu. Yesu Akawaambia. Asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kutwaa jiwe na kumtupia huyu mama mzinzi...Wote wakatawanyika....

    Anonymous said...

    Umesema vema sana mpendwa, ilihitaji uwajue au uende kwenye hivyo/au hao waimbaji ili uwaase hivyo na si kuwahukumu kama vile kuna mtu umemkamata akikuibia kihivyo.

    Ujue kuwa hata ndani ya wanafunzi wake Yesu kulikuwa na waharifu, lakini Yesu aliwavumilia. Kwa hiyo hao waimbaji ambao umewashutumu kwa kile unachosema hawafanani na kila wanachowaimbia/wahubiria wengine, lakini ni kwamba kwa njia hiyo huwasaidia wengine wali katika giza totoro na kumgeukia Mungu.

    Kama nyimbo zao ni baraka basi kuna faida ya mwimbaji regardless of how she/he is a sinner or whatever.Hakuna atakayekamilika mbele za Mungu mpaka siku yake mUNGU MWENYEWE IKAMILIKE.

    Waache waimbe maana wamesaidia wengi kunyoosha maisha yao.Yaache magugu yamee pamoja na ngano ili siku ya siku Mvunaji mwenyewe aje achambue.Tungekuwa tunafuata kila tendo la mtu asemacho tusingefika mbali maana hata wanasiasa wanaporojoa mengi tunawachagua na hawafanyi chochote na tena huja na mtindo uleule safari nyingine napo tunawachagua.

    Mwimbaji ni mtoa ujumbe tu, ukianza kuchambua maisha yake utajikuta wewe mchambuaji ndiye utaachwa soremba.Nakubaliana na wewe kwamba inabidi tuhubiri na kutenda sawasawa na mahubiri yetu ili tuwe nuru tosha kwa jamii inayopokea ujumbe wetu.Lakini suala la nmana hiyo libaki kwa uamuzi wa mtu mwenyewe pasipo mtu mwingine kumhukumu.
    Sisi wanadamu ni wenye dhambi tuliosamehewa na tunazidi kutenda dhambi kila kukicha ila Mungu ni mwenye huruma hutuhurumia na kutusamehe kila inayoitwa dakika.

    Binafsi nakushukuru kwa changamoto yako, lakini nakuasa usiikomalie kama vile wewe hauko duniani.