Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Lengo kuu la blogu ya nyimbozadini ni kuzikusanya video na audio mbalimbali za nyimbo za dini na kuziweka pamoja. Tunatumaini kwamba hii itawapunguzia shida ya kuhangaika kwenda katika mitandao mbalimbali kusaka video na audio hizi. Kwa hivyo video na nyimbo zote zilizopo hapa zinapatikana mtandaoni katika tovuti mbalimbali kama Youtube.com na Google videos. Nyimbozadini.Blogspot.Com haitunzi wala kuuza nyimbo zo zote na kama unataka kununua video za nyimbo utakazoziona hapa basi wasiliana na watoaji au wamiliki wa video hizo. Karibuni tuburudishe mioyo, roho na fikra zetu kwa nyimbo motomoto za Injili. Mungu Atubariki sana!!!
2 comments:
Bahati asante kwa ujumbe wako mzuri. Japo ndoa yako inapita katika misukosuko kutokana na kashfa ya mumeo kumpiga mimba mcheza sinema, numefurahishwa na jinsi ulivyokaa kimya na kujizuia. Usikimbilie talaka na bila shaka kitu chema kitachomoza katika msukosuko huu. Jifunze kutoka kwa Hillary Clinton na jinsi alivyosimama na mumewe katika wakati ule wa majaribu ya shetani. Roho mtakatifu akuongoze uendelee kutangaza injili ya Bwana. Tafadhali usije ukaiacha kazi hii. Ubarikiwe sana!
Mungu akubariki sana Bahati, huu wimbo unatia sana moyo hasa kwa mt ypyote ambaye amepitia majaribu maana kuna wakati kweli unaona kama Mungu hasikii uombapo! Kweli tumtegemee yeye na zadidi ya yote Yesu atuepushe na majaribu. Mungu akulinde na kukufunika mwana wake.
Post a Comment