(2) ZIPO FAIDA
(3) USINIPITE
(4) NAKUSHUKURU
(5) SITARUDI NYUMA
(6) MOYO WANGU
(7) YESU WANGU NI TUMAINI
(8) UNITETEE
(9) UINULIWE
Lengo kuu la blogu ya nyimbozadini ni kuzikusanya video na audio mbalimbali za nyimbo za dini na kuziweka pamoja. Tunatumaini kwamba hii itawapunguzia shida ya kuhangaika kwenda katika mitandao mbalimbali kusaka video na audio hizi. Kwa hivyo video na nyimbo zote zilizopo hapa zinapatikana mtandaoni katika tovuti mbalimbali kama Youtube.com na Google videos. Nyimbozadini.Blogspot.Com haitunzi wala kuuza nyimbo zo zote na kama unataka kununua video za nyimbo utakazoziona hapa basi wasiliana na watoaji au wamiliki wa video hizo. Karibuni tuburudishe mioyo, roho na fikra zetu kwa nyimbo motomoto za Injili. Mungu Atubariki sana!!!
5 comments:
Upendo Nkone at her best! Blessings
Nyimbo nzuri ajabu.
Lakini pengine macho yananidanganya. Inaonekana kama mtumishi wa Mungu AMEJICHUBUA kwani katika video zingine anaonekana mweupe. Namfahamu personally na ni pure chocolate. Kidogo natatanishwa na mtumishi wa Mungu KUJICHUBUA!!!
Duh! Unajua rangi ya asili hua inapendeza ajabu! Lakini sasa hapa mtumishi ukiweka mkono wako mwenyewe kwenye shavu lako mwenyewe watu wanaweza wakuambie, Hey, wewe, ondoa mkono wako kwenye shavu la mwenzio!!! Yani ni rangi mbili tofauti...!
Kwanza nampongeza sana dada Upendo Nkone kwa hatua kubwa aliyofikia. Kwa kweli mimi binafsi nyimbo zake zinanibariki kupita kiasi. Keep it up dada!
Kuhusiana na suala la rangi yake ya ngozi kuwa nyeupe, HAJAJICHUBUA. Ni rangi yake ya asili isipokuwa sehemu zinazoonekana nyeupe zaidi ni kutokana na kuathiriwa na taa za kuongeza mwanga kwenye upigaji wa picha za video.
Mpiga picha alitakiwa kubalance mwanga. Hata hivyo bado amependeza sana amevaa nguo za heshima zinazoendana na umbo lake. Inapendeza kwa kweli huku Ulaya kila mtu akiona DVD yake au kupitia kwenye blogu hii anamsifia sana unadhifu wake na uimbaji wake
Dada Upendo Mungu akubariki sana katika maisha yako yote, na vizazi vyako vyote, uwe na watoto wema watumishi, wasomi ili jina la BWANA YESU lizidi kuinuliwa na mataifa yote
Hata mimi nampenda sana dada Upendo Nkone...ila ukweli wa kujichubua....mtu aliyejichubua kuna mahali utaona tu, kwa mfano hwenye pingili za vidole, nk!
Hata hivyo...nampenda sana Upendo..ila nahisi amejichubua kidogo...ama labda kama ameacha sasa! Si kama nahukumu!
Post a Comment